Thursday, February 18, 2010

Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete na wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM wamesimama na kuinamisha vichwa, kumkumbuka aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM Mstaafu, Hayati Rashidi Mfaume Kawawa kabla ya kuanza kwa mkutano wao Mjini Dodoma Februari 13, 2010. Wengine pichani kutoka kushoto ni Mwenyekiti Mstaafu wa CCM na Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa, Mwenyekiti Mstaafu na Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi , Makamu mwenyekiti wa CCM (Zanzibar), Aman Abeid Karume, Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) , Pius Msekwa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

kamati kuu ya CCM Feb 13, 2010, Dodoma

Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete na wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM wamesimama na kuinamisha vichwa, kumkumbuka aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM Mstaafu, Hayati Rashidi Mfaume Kawawa kabla ya kuanza kwa mkutano wao Mjini Dodoma Februari 13, 2010. Wengine pichani kutoka kushoto ni Mwenyekiti Mstaafu wa CCM na Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa, Mwenyekiti Mstaafu na Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi , Makamu mwenyekiti wa CCM (Zanzibar), Aman Abeid Karume, Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) , Pius Msekwa.

SULEIMANI NYAMBUI NA MBIO ZA NYIKA 2010

Katibu Mkuu wa Chama cha Riadha Tanzania(RT) Suleiman Nyambui (kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari jijini hivi karibuni kuhusu wakimbiaji wa mbio za nyika za Kilimanjaro 2010 ambazo zitafanyika mwisho wa mwezi huu Mkoani Kilimanjaro(kulia) ni Meneja wa Bia ya Kilimanjaro George Kavishe.Mbio hizo za nyika zimedhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro, Vodacom.pamoja na makampuni mengine nchini ikiwemo kampuni ya KK Security,Tanga Cement.Good Year, Kilimanjaro Water,Tanzanite One, DT Dobie Tanzania, TPC, New Africa Hotel na Keys Hotel. Picha na Mwanakombo Jumaa.-Maelezo